Kanuni za Sumatra

Kanuni ya 18 ya Sheria za SUMATRA[GN] No.218/2007 Vitendo Vinavyokatazwa.

 Wafanyakazi katika gari la abiria, wakiwa kazini Wasifanye vitendo  vifuatavyo:-

 1.   Hairuhusiwi kutumia lugha chafu ya uhasama au  matusi kwa abiria .
 2. Hairuhusiwi kuwaziba au kuwazuia kwa makusudi wahudumiaji wengine
 3. Hairuhusiwi kuendesha gari zaidi ya vikomo vya spidi  kwa kushindania     abiria.
 4.  Hairuhusiwi kukatisha safari kabla ya kufika kituo cha mwisho.
 5. Hairuhusiwi kuendesha gari la abiria akiwa amekunywa  pombe au kutumia  madawaya kulevya kiasi  chochote  kile.
 6. Hairuhusiwi kuendesha gari la abiria kwa uzembe au namna ya hatari au kinyume na  sheria ya Usalama barabaranina sheria nyinginezo.
 7.   Hairuhusiwi kubughudhi au kusumbua abiria.
 8.  Hairuhusiwi kubugudhi au kusumbua wanafunzi.
 9.  Hairuhusiwi kuendesha gari la abiri hali dereva anazungumza na  simu za kiganjani.
 10. Hairuhusiwi kupakia   wanyama hai au vitu vya hatari  kwenye  gari la abiria.

Mmiliki wa leseni ya gari la abiria au  mtumishi wake ambae atavunja au
kushindwa kutekeleza kanuni ndogo ya [1]  atakuwa anatenda kosa la jinai
na anapaswa, kutiwa hatiani, kutozwa faini isiyo chini ya shilingi laki tano,
au kufungwa jela kwa muda usiopungua  mwaka mmoja na usiozidi miaka
miwili, au kutozwa faini na kufungwa jela.

Kanuni ya 22 ya Sheria za SUMATRA [GN] No.218/2007  Kuharibika Kwa Gari  La Abiria.

Ikiwa kutokana na gari la abiria kuharibika au gari hilo haliko katika hali  ya kuanza au kuendelea na safari, mmiliki wa leseni ya au mfanyakazi wake lazima-:

 1. Liondolewe barabarani.
 2. Abiria ana haki ya kupata usafiri mbadala ndani ya muda wa  dakika kumi au warudishiwe nauli: na
 3.  Kwa gari la abiria litoalo huduma kati ya mji na mji litengenezwe  ndani ya muda  usiozidi masaa.

Ikiwa baada ya matengenezo ya gari la abiria kwa mujibu wa kanuni   ndogo ya 1[b]  gari hilo bado haliko katika hali ya kuanza au   kuendelea na safari, mmiliki wa leseni au mfanyakazi lazima atoe usafiri mbadala.

Kanuni ya 23 ya Sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Haki ya Kulipia Mizigo.
1.    Abiria ana haki bila malipo kubeba mzigo wenye uzito wa kilo ishirini na mtoto mzigo wenye uzito wa kilo kumi.

2.    Abiria akibeba mzigo zaidi ya ule anaoruhusiwa kubebwa bila malipo, mmiliki wa leseni ya gari la abiria ana haki ya kumtoza abiria huyo  malipo kwa kilo ya ziada kwa mujibu wa viwango vilivyoruhusiwa.

Kanuni ya 24 ya Sheria za  SUMATRA [GN]  No.218/2007 Haki ya Kufuta Oda na  Kurudishiwa Nauli.
1.    Abiria ana haki ya kufuta oda yake ya safari kabla ya kuanza safari.

2.    Abiria ana haki ya kurudishiwa nauli hiyo baada ya kufuta oda yake ya safari masaa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa kuanza safari ya  gari la abiria.

3. Abiria ana haki ya kurudishiwa nauli hiyo baada ya kukatwa asilimia kumi na tano ya nauli hiyo endapo oda ya safari itafutwa ndani ya muda unaopungua masaa ishirini  nne na kabla ya muda uliopangwa.

Kanuni ya 25 ya sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Haki ya Kupewa Tiketi.
Kwa gari la abiria litoalo huduma kati ya mji na  mji

 1. Abiria ana haki ya kupewa tiketi yenye jina  lake pamoja na namba  ya kiti chake.
 2. Abiria ana haki ya kufahamu muda wa kuwasili kituoni  na kuanza
  safari.
 3. Abiria ana haki ya kufahamu kituo aendacho.
 4. Abiria  ana haki ya kufahamu tarehe ya  safari.
 5. Abiria ana haki ya kufahamu namba ya usajili ya gari  hilo la abiria.
 6. Abiria ana haki ya kufahamu nauli ya safari hiyo.
 7. Abiria ana haki ya kufahamu anuani na namba ya simu ya mmiliki wa leseni.
 8. Abiria ana haki ya kufahamu namba za usajili wa gari hilo.
 9. Abiria ana haki ya kufahamu jina la njia ihudumiwayo.
 10. Abiria ana haki ya kufahamu tarehe ya kutolewa tiketi na tarehe ya safari; na
 11. Abiria ana haki ya kufahamu namba mfululizo ya tiketi.

Kwa huduma za usafiri ndani ya mji,mmiliki wa gari la abiria atatoa tiketi
zilizochapishwa ambazo zitaonyesha namba ya usajili wa gari lenye leseni,
njia, nauli iliyoidhinishwa, jina na anuani ya mwenye gari au mmiliki wake
na tarehe ya kutolewa
.

Kanuni ya 26 ya sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Nauli za Watoto na Wanafunzi.
Kwa usafiri wa mjini, kila mtoto na mwanafunzi atakaepanda gari la abiria atakua na haki ya kusafiri kwa kulipa nusu ya nauli anayotozwa mtu mzima kwa safari hiyo hiyo.

Powered by BIDC