Haki za Abiria

HAKI ZA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA USAFIRISHAJI ZA MWAKA 2007 GN.218/2007

 1. Haki ya kurudishiwa nauli chombo cha usafiri kinapochelewa kuanza safari saa mbili baada ya muda uliopangwa kwenye ratiba na tiketi (Kanuni No. 21-(2) ).
 2. Haki ya kupewa tiketi ndani ya ofisi ya mtoa huduma ya usafiri husika na siyo vinginevyo (Kanuni ya 17-(1p) na ya 24-(1) ).
 3. Haki ya kutonyanyaswa kwa lugha za matusi au vitendo vyovyote kinyume na taratibu au kwa mujibu wa haki za binadamu iwe kwa abiria mtu mzima au mwanafunzi (Kanuni ya 18-(1a,g,h) ).
 4. Haki ya kufikishwa mwisho wa safari yaani kituo husika anakoelekea abiria (Kanuni ya 18-(1d) ).
 5. Haki ya kutosimamishwa ndani ya chombo cha usafiri (kwa mabasi ya mikoani) awapo safarini (Kanuni 17-1f) ).
 6. Haki ya kulipa nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka ya SUMATRA na si zaidi ya kiwango husika (Kanuniya 34-1,2,3) ).
 7. Haki ya kutoendeshwa na dereva mmoja (kwa mabasi ya mikoani) zaidi ya saa nane (Kanuni ya 17-1g).
 8. haki ya kulindwa kwa mikanda ya usalama (Passengers seat belt) wakati wote wa safari (Kanuni ya 17-1i).
 9. Haki ya kupata huduma muhimu za usafi, afya na taarifa zinazohusiana na safari yake (Kanuni ya 17-1l,m,n).
 10. Haki ya kutolipia mzigo usiozidi kilogramu ishirini kwa mtu mzima na kilogramu kumi kwa mtoto (Kanuni ya 23-1,2).
 11. Haki ya kurudishiwa nauli yote abiria pale anapohailisha safari saa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa safari wa chombo husika kama ilivyoainishwa kwenye tiketi na ratiba (Kanuni ya 24-1,2,3).
 12. Haki ya kuhifadhiwa/kutunziwa vifaa au mali ya abiria vinapothibitishwa kusahaulika ndani ya chombo cha usafiri husika (Kanuni ya 38).
 13. Haki ya kurudishiwa nauli pungufu ya asilimia kumi na tano tu ya kiasi alicholipa kama ilivyoainishwa kwenye tiketi endapo abiria atavunja safari ndani ya muda chini ya saa ishirini na nne kabla ya muda wa chombo cha usafiri kuanza safari (Kanuni ya 24-3).

Kanuni ya 18 ya Sheria za SUMATRA [GN] No.218/2007 Vitendo Vinavyokatazwa.

 Wafanyakazi katika gari la abiria, wakiwa kazini Wasifanye vitendo vifuatavyo-:

 1.   Hairuhusiwi kutumia lugha chafu ya uhasama au  matusi kwa abiria .
 2.  Hairuhusiwi kuwaziba au kuwazuia kwa makusudi wahudumiaji wengine wa usafiri
 3. Hairuhusiwi kuendesha gari zaidi ya vikomo vya spidi  kwa kushindania abiria.
 4. Hairuhusiwi kukatisha safari kabla ya kufika kituo cha mwisho.
 5. Hairuhusiwi kuendesha gari la abiria akiwa amekunywa  pombe au kutumia  madawa ya kulevya kiasi    chochote  kile.
 6. Hairuhusiwi kuendesha gari la abiria kwa uzembe au namna ya hatari au kinyume na  sheria ya Usalama barabaranina sheria nyinginezo.
 7. Hairuhusiwi kubughudhi au kusumbua abiria.
 8.  Hairuhusiwi kubugudhi au kusumbua wanafunzi.
 9.  Hairuhusiwi kuendesha gari la abiri hali dereva anazungumza na simu za kiganjani.
 10. Hairuhusiwi kupakia   wanyama hai au vitu vya hatari  kwenye gari la abiria.

Mmiliki wa leseni ya gari la abiria au  mtumishi wake ambae atavunja au kushindwa kutekeleza kanuni ndogo ya [1]  atakuwa anatenda kosa la jinai na anapaswa, kutiwa hatiani, kutozwa faini isiyo chini ya shilingi laki tano,au kufungwa jela kwa muda usiopungua  mwaka mmoja na usiozidi miaka miwili, au kutozwa faini na kufungwa jela.

Kanuni ya 22 ya Sheria za SUMATRA [GN] No.218/2007  Kuharibika Kwa Gari  La Abiria.

 Ikiwa kutokana na gari la abiria kuharibika au gari hilo haliko katika ha ya kuanza au kuendelea na safari, mmiliki wa leseni ya au mfanyakazi wake lazima-:

 1. Liondolewe barabarani.
 2. Abiria ana haki ya kupata usafiri mbadala ndani ya muda wa dakika kumi au warudishiwe nauli: na
 3. Kwa gari la abiria litoalo huduma kati ya mji na mji litengenezwe  ndani ya muda  usiozidi masaa.

Ikiwa baada ya matengenezo ya gari la abiria kwa mujibu wa kanuni ndogo ya 1[b]  gari hilo bado haliko katika hali ya kuanza au  kuendelea na safari, mmiliki wa leseni au mfanyakazi lazima atoe usafiri mbadala.

Kanuni ya 23 ya Sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Haki ya Kulipia Mizigo.

 1.   Abiria ana haki bila malipo kubeba mzigo wenye uzito wa kilo ishirini na mtoto mzigo wenye uzito wa kilo kumi.
 2.  Abiria akibeba mzigo zaidi ya ule anaoruhusiwa kubebwa bila malipo, mmiliki wa leseni ya gari la abiria ana haki ya kumtoza abiria huyo    malipo kwa kilo ya ziada kwa mujibu wa viwango vilivyoruhusiwa.

Kanuni ya 24 ya Sheria za  SUMATRA [GN]  No.218/2007 Haki ya Kufuta Oda na  Kurudishiwa Nauli.

 1. Abiria ana haki ya kufuta oda yake ya safari kabla ya kuanza safari.
 2. Abiria ana haki ya kurudishiwa nauli hiyo baada ya kufuta oda yake ya safari masaa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa kuanza safari ya gari la abiria.
 3.  Abiria ana haki ya kurudishiwa nauli hiyo baada ya kukatwa asilimia kumi na tano ya nauli hiyo endapo oda ya safari itafutwa ndani ya muda unaopungua masaa ishirini  nne na kabla ya muda uliopangwa.

 Kanuni ya 25 ya sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Haki ya Kupewa Tiketi.
 Kwa gari la abiria litoalo huduma kati ya mji na  mji

 1.  Abiria ana haki ya kupewa tiketi yenye jina  lake pamoja na namba  ya kiti chake.
 2.   Abiria ana haki ya kufahamu muda wa kuwasili kituoni  na kuanza safari.
 3. Abiria ana haki ya kufahamu kituo aendacho.
 4. Abiria  ana haki ya kufahamu tarehe ya  safari.
 5.  Abiria ana haki ya kufahamu namba ya usajili ya gari  hilo la abiria.
 6. Abiria ana haki ya kufahamu nauli ya safari hiyo.
 7. Abiria ana haki ya kufahamu anuani na namba ya simu ya mmiliki wa leseni.
 8. Abiria ana haki ya kufahamu namba za usajili wa gari hilo.
 9. Abiria ana haki ya kufahamu jina la njia ihudumiwayo.
 10. Abiria ana haki ya kufahamu tarehe ya kutolewa tiketi na tarehe ya safari; na
 11. Abiria ana haki ya kufahamu namba mfululizo ya tiketi.

Kwa huduma za usafiri ndani ya mji,mmiliki wa gari la abiria atatoa tiketi
zilizochapishwa ambazo zitaonyesha namba ya usajili wa gari lenye leseni,
njia, nauli iliyoidhinishwa, jina na anuani ya mwenye gari au mmiliki wake na tarehe ya kutolewa.

 Kanuni ya 26 ya sheria za SUMATRA [GN] No. 218/2007 Nauli za Watoto na Wanafunzi. 
Kwa usafiri wa mjini, kila mtoto na mwanafunzi atakaepanda gari la abiria atakua na haki ya kusafiri kwa kulipa nusu ya nauli anayotozwa mtu mzima kwa safari hiyo hiyo.


 

 


Powered by BIDC